Nadharia
Nadharia (kutoka neno la Kiarabu; kwa Kiingereza: "theory") ni mkusanyo wa taarifa mbalimbali zenye ukweli ndani yake bila kuegemea upande fulani.
Katika lugha nyingi za Ulaya, neno hili asili yake ni katika Kigiriki cha kale lakini kwa matumizi ya kisasa imechukua maana kadhaa zenye kuhusiana nalo.
Nadharia zinaongoza shughuli za kupata ukweli badala ya kufikia malengo, na huwa haiegemei upande wowote. Nadharia inaweza kuwa jumla ya ujuzi ambao unaweza au usiweze kuambatana na mafunzo ya kimatendo. Kuunda nadharia ni kutengeneza ujuzi.
Makala hii kuhusu mambo ya elimu bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Nadharia kama historia yake, uenezi au maendeleo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |