Polokwane
Polokwane (kwa Kiafrikaans: Pietersburg) ni manisipaa ya Afrika Kusini na mji mkuu wa Jimbo la Limpopo. Mji una wakazi nusu milioni.
Jiji la Polokwane | |
Mahali pa mji wa Polokwane katika Afrika Kusini |
|
Majiranukta: 23°53′24″S 29°27′0″E / 23.89000°S 29.45000°E | |
Nchi | Afrika Kusini |
---|---|
Majimbo | Limpopo |
Idadi ya wakazi | |
- Wakazi kwa ujumla | 123,749 |
Tovuti: www.polokwane.org.za |
Historia
haririMji ulianzishwa mwaka 1886 na makaburu wa Voortrekker ukapewa jina la Pietersburgh kwa heshima ya jenerali ya makaburu Petrus Jacobus "Piet" Joubert. Wakati wa Vita ya pili ya Waingereza dhidi ya Makaburu Pietersburgh ikawa mji mkuu wa jamhuri ya Transvaal ikavamiwa na Waingereza mwaka 1901.
Jiografia
haririPolokwane iko katika nyanda za juu kwa kimo cha mita 1,312. Hali ya hewa ni ya wastani yenye sentigredi 27°C wakati wa joto na 20°C wakati wa baridi.
Uchumi
haririKuna migodi ya almasi na kiwanda cha kuchimbia mchanga safi sana unaofaa matumizi ya vioo. Pamoja na migodi kuna pia viwanda mbalimbali.
Michezo
haririPolokwane iliona michezo ya mpira wakati wa kombe la dunia la 2010. Polokwane pia ni jina la timu ya mpira wa miguu, na ndiyo makao makuu ya timu hiyo ijulikanayo kama "Polokwane Football Club"
Viungo vya Nje
hariri- Tovuti rasmi Archived 4 Februari 2010 at the Wayback Machine.
Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika Kusini bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Polokwane kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |