Quebec (Kiingereza: Quebec, Kifaransa: Québec) ni jimbo la Kanada upande wa Bahari Atlantiki kati ya mdomo wa mto Saint Lawrence hadi ghuba ya Hudson. Imepakana na Ontario, New Brunswick na Newfoundland and Labrador.

Quebec

Bendera

Nembo
Nchi Bendera ya Kanada Kanada
Mji mkuu Jiji la Quebec
Eneo
 - Jumla 1.365.128 km²
Tovuti:  http://www.quebec.ca/
Msitu wa Gaspé, Québec
Ramani ya Quebec

Ina eneo la km² 1,542,056 ikiwa ni kubwa zaidi kati ya majimbo ya Kanada.

Kuna wakazi milioni saba na nusu (7,546,131).

Quebec ni eneo ambako wakazi wengi hutumia lugha ya Kifaransa, tofauti na majimbo mengine ya Kanada ambako watu huongea Kiingereza. Sababu yake ni kwamba sehemu hii ilikuwa koloni la Ufaransa tangi karne ya 17 na walowezi Wafaransa walijenga makazi yao hapa. Walitunza utamaduni wao hata baada ya vita ya miaka saba (1756-1762) ambako koloni ilivamiwa na Uingereza na kuwa eneo la Kiingereza. Mfaransa wa kwanza aliyefika Quebec alikuwa mpelelezi Jacques Cartier.

Quebec ilikuwa na harakati mbalimbali zilizolenga kujitenga kwa Quebec katika Kanada na kuunda nchi mpya. Katika kura ya wananchi ya mwaka 1995 azimio la kubaki ndani ya Kanada lilichukuliwa kwa kura chache sana; 49.4% za wananchi wa Quebec walipendelea kuondoka katika Kanada na 50.6% walipendelea kubaki ndani ya Kanada.

Mji mkuu ni Jiji la Quebec ambayo ni kati ya miji ya kale ya Amerika ya Kaskazini. Mji mkubwa wa jimbo na mji wa pili wa Kanada ni Montreal.

Miji Mikubwa

hariri
  1. Montreal (1.620.693)
  2. Jiji la Quebec (491.142)
  3. Laval (368.709)
  4. Gatineau (242.124)

Viungo vya nje

hariri
 
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
  Makala hii kuhusu maeneo ya Kanada bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Quebec kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.