Tenzing Norgay
Tenzing Norgay (Mei 1914 – 9 Mei 1986) alikuwa sherpa kutoka nchi ya Nepal aliyekuwa pamoja na Edmund Hillary mtu wa kwanza kukanyaga kilele cha Mlima Everest tarehe 29 Mei 1953.
Maisha
haririAlikuwa mtoto wa wakulima maskini aliyezaliwa wakati wa kuhiji kwa wazazi wake huko Tibet.
Akiwa kijana alianza kazi ya kuongoza watalii na wapanda milima jinsi walivyofanya wanaume wengi wa kabila lake.
Akiongozana na misafara kwenye milima ya Himalaya tangu mwaka 1935 alijaribu mara kadhaa kupanda mlima Everest bila kufaulu.
Mwishowe akiongozana na Edmund Hillary walifika kwenye kilele katika msafara wa Mei 1953.
Kwa miaka mingi watu kutoka Asia na Ulaya walivutana kuhusu swali kama Tenzing au Hillary alikuwa mtu wa kwanza wa kufika kileleni. Wote wawili wakiwa marafiki wakajibu ya kwamba walifika pamoja bila kubagua nani alikuwa mbele hatua chache.
Baadaye mwana na mjukuu wa Tenzing walifika pia kwenye kilele cha Everest.
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Tenzing Norgay kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |