Venezuela
Venezuela ni nchi kaskazini mwa Amerika ya Kusini.
| |||||
Kaulimbiu ya taifa: None 2 | |||||
Wimbo wa taifa: Gloria al Bravo Pueblo | |||||
Mji mkuu | Caracas | ||||
Mji mkubwa nchini | Caracas | ||||
Lugha rasmi | Kihispania 3 | ||||
Serikali | Shirikisho la jamhuri Nicolás Maduro | ||||
Uhuru Kutoka Hispania Kutoka Gran Colombia ilitambuliwa |
5 Julai 1811 21 Novemba 1831 30 Machi 1845 | ||||
Eneo - Jumla - Maji (%) |
916,445 km² (ya 33) 0.32 | ||||
Idadi ya watu - 2015 kadirio - 2001 sensa - Msongamano wa watu |
33,221,865 (ya 44) 23,054,210 30.2/km² (ya 175) | ||||
Fedha | Bolivar (VEB )
| ||||
Saa za eneo - Kiangazi (DST) |
AST (UTC-4) None (UTC) | ||||
Intaneti TLD | .ve | ||||
Kodi ya simu | +58
- | ||||
1 Jamhuri ya Kibolivari ya Venezuela imekuwa jina la nchi tangu katiba ya 1999. "Kibolivar" ni jina la heshima kwa kumbukumbu ya mshujaa wa uhuru Simon Bolivar. 2 Zamani: Dios y Federación ("Mungu na Shirikisho") 3 Katiba inatambua pia lugha asilia zote nchini. |
Imepakana na Brazil, Guyana na Kolombia.
Mbele ya pwani ya Bahari ya Karibi kuna madola ya visiwani ya Aruba, Antili za Kiholanzi na Trinidad na Tobago.
Venezuela ilikuwa koloni la Hispania hadi mwaka 1811 na lugha ya Kihispania ni lugha ya kitaifa.
Kikatiba Venezuela ni shirikisho la jamhuri.
Asili ya jina "Venezuela"
haririJina la nchi ni umbo la Kihispania la jina la mji wa Venezia (Italia). Amerigo Vespucci, mpelelezi Mwitalia katika utumishi wa mfalme wa Hispania, aliona vijiji vya wenyeji waliojenga nyumba juu ya maboriti yaliyosimamishwa katikati ya maji karibu na mwambao pasipo kina. Vijiji vilimkubusha mji wa Venezia uliojengwa vilevile. Venezuela yamaanisha "Venezia Ndogo" katika Kihispania.
Jiografia
haririVenezuela ina eneo la km² 916,445 (kama Namibia) ikiwa na pwani yenye urefu wa km 2,800. Asilimia 39 za eneo hili ni misitu, mashamba ya kulimwa ni 4%, eneo la mifugo 20%, mazao ya kudumu kama kahawa 1%.
Kuna kanda nne za kijiografia:
- tambarare za pwani karibu na Maracaibo katika kaskazini-magharibi
- milima ya Andes
- tambarere za mto Orinoko katikati ya nchi
- nyanda za juu za Guayana katika kusini-mashariki
Milima ya meza
haririNyanda za juu za Guayana zina milima ya pekee: kuna milima ya meza 115 inayoitwa "tepui" katika lugha ya wakazi asilia. Kiekolojia hilo ni eneo muhimu kwa sababu milima mingi ina mimea na wanyama wa pekee, tofauti na milima jirani, na inapatikana hapa tu kote duniani.
Maporomoko marefu duniani yatelemka kutoka milima hii kama vile maporomoko ya Salto del Angel ("anguko la malaika") ambako maji huanguka mita 965.
Mito
haririMto mkubwa wa Venezuela ni Orinoco wenye urefu wa km 2574 unaoishia katika Atlantiki. Lakini mkono wa Brazo Casiquiare unajitenga na kuishia katika mto wa Amazonas nchini Brazil.
Matawimto muhimu ya Orinoco ni Rio Apure na Rio Caroni.
Majimbo katika shirikisho
hariri- Tazama pia Majimbo ya Venezuela
Venezuela ni shirikisho la madola au majimbo 23 ya kujitawala, maeneo yasiyojitawala na mkoa wa shirikisho wa Caracas.
Jimbo | Mji Mkuu | Wakazi | Eneo | Kanda | |
---|---|---|---|---|---|
Amazonas | Puerto Ayacucho | 70,464 | 180,144 km² | Guayana | |
Anzoátegui | Barcelona | 1,222,225 | 43,300 km² | Nor - Oriental | |
Apure | San Fernando de Apure | 377,756 | 76,500 km² | Llanos | |
Aragua | Maracay | 1,449,616 | 7,014 km² | Central | |
Barinas | Barinas | 624,508 | 35,200 km² | Andean | |
Bolívar | Ciudad Bolívar | 1,214,846 | 238.000 km² | Guayana | |
Carabobo | Valencia | 1,932,168 | 4,650 km² | Central | |
Cojedes | San Carlos | 253,105 | 14,800 km² | Central | |
Delta Amacuro | Tucupita | 97,987 | 40,200 km² | Guayana | |
Falcón | Coro | 763,180 | 24,800 km² | Central - Occidental | |
Guárico | San Juan de los Morros | 627,086 | 64,986 km² | Llanos | |
Lara | Barquisimeto | 1,556,415 | 19,800 km² | Central - Occidental | |
Mérida | Mérida | 715,268 | 11,300 km² | Andean | |
Miranda | Los Teques | 2,330,872 | 7,950 km² | Capital | |
Monagas | Maturín | 712,626 | 28,930 km² | Nor - Oriental | |
Nueva Esparta | La Asunción | 712,626 | 1,150 km² | Insular | |
Portuguesa | Guanare | 725,740 | 15,200 km² | Central - Occidental | |
Sucre | Cumaná | 786,483 | 11,800 km² | Nor - Oriental | |
Táchira | San Cristóbal | 992,669 | 11,100 km² | South - Occidental | |
Trujillo | Trujillo | 608,563 | 7,400 km² | Andean | |
Vargas | La Guaira | 298,109 | 1,496 km² | Capital | |
Yaracuy | San Felipe | 499,049 | 7,100 km² | Central - Occidental | |
Zulia | Maracaibo | 2,983,679 | 63,100 km² | Zulian | |
Dependencias Federales (maneo chini ya shirikisho) | - | 2,245 | 342 km² | Insular (visiwa) | |
Distrito Federal Caracas (Mkoa wa shirikisho) | - | 2,284,921 | 433 km² | Capital (mji mkuu) |
Watu
haririWakazi wengi (51.6%) wanajiainisha kama machotara wa Kizungu-Kiindio. Wazungu ni 43.6%, wenye asili ya Afrika ni 3.5% na Waindio 2.6%. Utafiti wa DNA unaonyesha kwamba urithi wa jeni kwa asilimia 60.6 ni wa Kizungu, 23 ni wa Kiindio na 16.3 ni wa Kiafrika.
Lugha rasmi na ya kawaida ni Kihispania, ingawa lugha asilia zinakubalika kwa Waindio, na lugha nyingine zinatumiwa na wahamiaji.
Upande wa dini, 88% ni Wakristo, hasa wa Kanisa Katoliki (71%) na madhehebu mbalimbali ya Uprotestanti (17%).
Tazama pia
haririViungo vya nje
hariri- (Kihispania) Serikali ya Venezuela tovuti rasmi Archived 25 Juni 2001 at the Wayback Machine.
- (Kiingereza) Venezuela entry at The World Factbook
- (Kiingereza) Venezuela Archived 7 Juni 2008 at the Wayback Machine. at UCB Libraries GovPubs
- (Kiingereza) Venezuela katika Open Directory Project
- (Kiingereza) Venezuela from the Library of Congress Country Studies (1990)
- (Kiingereza) Venezuela profile from the BBC News
- (Kiingereza) Maps on Venezuela – Cartographic features Archived 16 Januari 2013 at the Wayback Machine.
- (Kiingereza) Key Development Forecasts for Venezuela from International Futures
- (Kiarabu) Venezuela and Tourism Archived 18 Desemba 2013 at the Wayback Machine. from Sky Immigration
- Wikimedia Atlas of Venezuela
Nchi na maeneo ya Amerika Kusini |
Argentina | Bolivia | Brazil | Chile | Ekuador | Guyana | Guyani ya Kifaransa | Kolombia | Paraguay | Peru | Surinam | Uruguay | Venezuela |
Makala hii kuhusu maeneo ya Amerika Kusini bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Venezuela kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |