Tanuri (kundinyota) : Tofauti kati ya masahihisho
No edit summary |
Add 1 book for verifiability (20211002sim)) #IABot (v2.0.8.1) (GreenC bot |
||
Mstari 11: | Mstari 11: | ||
Chaguo la jina lilikuwa dalili ya kipindi cha [[Zama za Mwangaza]] ambako Lacaille alitumia majina ya zana za siku zake kwa kutaja nyota, si tena majina ya [[mitholojia]] ya kale. |
Chaguo la jina lilikuwa dalili ya kipindi cha [[Zama za Mwangaza]] ambako Lacaille alitumia majina ya zana za siku zake kwa kutaja nyota, si tena majina ya [[mitholojia]] ya kale. |
||
Tanuri imepokelewa kati ya makundinyota 88 yanayoorodheshwa na [[Umoja wa kimataifa wa astronomia]] <ref>[https://www.iau.org/public/themes/constellations/ The Constellations], tovuti ya International Astronomical Union , iliangaliwa Julai 2017</ref> kwa jina la Fornax. Kifupi chake rasmi kufuatana na [[Ukia]] ni 'For'.<ref name="pa30_469">{{cite journal | last=Russell | first=Henry Norris | title=The New International Symbols for the Constellations | journal=[[Popular Astronomy (US magazine)|Popular Astronomy]] | volume=30 | pages=469–71 | bibcode=1922PA.....30..469R | year=1922}}</ref> |
Tanuri imepokelewa kati ya makundinyota 88 yanayoorodheshwa na [[Umoja wa kimataifa wa astronomia]] <ref>[https://www.iau.org/public/themes/constellations/ The Constellations], tovuti ya International Astronomical Union , iliangaliwa Julai 2017</ref> kwa jina la Fornax. Kifupi chake rasmi kufuatana na [[Ukia]] ni 'For'.<ref name="pa30_469">{{cite journal | last=Russell | first=Henry Norris | title=The New International Symbols for the Constellations | url=https://archive.org/details/sim_popular-astronomy_1922-10_30_8/page/469 | journal=[[Popular Astronomy (US magazine)|Popular Astronomy]] | volume=30 | pages=469–71 | bibcode=1922PA.....30..469R | year=1922}}</ref> |
||
==Nyota== |
==Nyota== |
Pitio la 17:53, 2 Oktoba 2021
Tanuri (kwa Kilatini na Kiingereza Fornax) [1] ni jina la kundinyota ndogo kwenye nusutufe ya kusini ya Dunia yetu.
Mahali pake
Tanuri lipo jirani na makundinyota ya Nahari (Eridanus) upande wa mashariki, kaskazini na kusini, ilhali Ketusi (Cetus), Najari (Sculptor) na Zoraki (Phoenix) ziko upande wa magharibi.
Jina
Tanuri ni kati ya makundinyota yaliyobuniwa katika enzi ya kisasa. Kama nyota nyingine zinazoonekana kutoka nusutufe ya kusini pekee haikujulikana kwa Wagiriki wa Kale wala kwa Waarabu kwa hiyo wataalamu wa Ulaya hawakuwa na habari nazo. Kundinyota hili lilielezwa mara ya kwanza na Mfaransa Nicolas-Louis de Lacaille wakati wa karne ya 18 kwa jina “Fourneau Chymique“ lililomaanisha “Tanuri ya kikemia“ yaani tanuri jinsi ilivyotumiwa kwa kuyeyusha metali kwa utafiti wa aloi na kampaundi.
Lacaille alikaa miaka miwili kwenye Rasi ya Tumaini Jema (Afrika Kusini) alipotazama nyota za anga la kusini ambazo wakati ule zilianza tu kujulikana kati ya wanaastronomia wa Ulaya. Hapo alipima nyota 10,000 na kuzipanga kwa makundinyota na kutunga majina kwa makundinyota mapya 14[2]. Jina la Kifaransa lilitafsiriwa kwa Kilatini na kufupishwa kama "Fornax“(Tanuri). Chaguo la jina lilikuwa dalili ya kipindi cha Zama za Mwangaza ambako Lacaille alitumia majina ya zana za siku zake kwa kutaja nyota, si tena majina ya mitholojia ya kale.
Tanuri imepokelewa kati ya makundinyota 88 yanayoorodheshwa na Umoja wa kimataifa wa astronomia [3] kwa jina la Fornax. Kifupi chake rasmi kufuatana na Ukia ni 'For'.[4]
Nyota
Nyota za Tanuri ni chache na dhaifu; kuna nyota 59 zenye mwangaza unaoonekana wa mag 6.5 hivyo zinaonekana kwa macho matupu mahali penye giza. [5] lakini hakuna iliyo angavu kushinda mag 3 [6].
Nyota tatu angavu zaidi ni Alfa, Beta na Nu Fornacis zinazofanza pembetatu bapa. Nyota sita zilitambuliwa kuwa na sayari za nje.
Alfa Fornacis ina mag 3.91 ni nyota maradufu inayoweza kutambuliwa vile kwa msaada wa darubini ndogo. Ina umbali wa miaka nuru 46 kutoka Dunia.
Jina la (Bayer) |
Namba ya Flamsteed |
Jina (Ukia) |
Mwangaza unaoonekana |
Umbali (miaka nuru) |
Aina ya spektra |
---|---|---|---|---|---|
α | *[7] | Dalim, Fornacis | 3,80m | 40 | F7 + G7 |
β | 4,45m | 200 | G7 III | ||
ν | 4,45m | ||||
Tanbihi
- ↑ Uhusika milikishi (en:genitive) ya neno "Fornax " katika lugha ya Kilatini ni "Fornacis" na hili ni umbo la jina linaloonekana katika majina ya nyota za kundi hili kama vile Alfa Fornacis, nk.
- ↑ Histoire de l'Académie royale des sciences ; taarifa ya Lacaille katika "Historia ya Akademia ya Kifalme ya sayansi", uk. 588, Tovuti ya Bibliothèque nationale de France (BnF), iliangaliwa Julai 2017
- ↑ The Constellations, tovuti ya International Astronomical Union , iliangaliwa Julai 2017
- ↑ Russell, Henry Norris (1922). "The New International Symbols for the Constellations". Popular Astronomy. 30: 469–71. Bibcode:1922PA.....30..469R.
- ↑ The Bortle Dark-Sky Scale
- ↑ Fornax kwenye tovuti ya Ian Ridpath « Star Tales »
- ↑ 12 Eri
Viungo vya Nje
Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Tanuri (kundinyota) kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |