Nenda kwa yaliyomo

Batman

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Pitio kulingana na tarehe 23:18, 15 Januari 2021 na InternetArchiveBot (majadiliano | michango) (Rescuing 1 sources and tagging 0 as dead.) #IABot (v2.0.8)
(tofauti) ← Pitio lililotangulia | Toleo la sasa (tofauti) | Pitio linalofuata → (tofauti)
Mji wa Batman.

Batman (kifupi cha Milima ya Batı Raman) ni jina la mji mkuu wa Mkoa wa Batman, katika Uturuki. Mji huo pia unajulikana kwa jina la Kikurdi Êlih au Iluh.[1] Ni mji ulioko katika Mto Batman ambao unajulikana sana kwa jina la Kikurdi kusini-mashariki mwa nchi ya Uturuki.[2]

Mkoa wa Batman ni eneo muhimu kabisa la uzalishaji wa mafuta, na mji wa Batman una maeneo ya kale ya vifaa vya kale vya kuchimbia mafuta, ambavyo vilianzishwa tangu mwaka wa 1955.

Kuna takriban km 494 (mi 307) za bomba la kupitishia mafuta kutoka mjini Batman kuelekea İskenderun. Kuna njia ya reli iliyo karibu kidogo na Kurtalan ambayo imeunganisha njia hiyo hadi kutoka katika mji wa Istanbul. Katika mji wa Batman, pia kuna uwanja wa ndege wa mkoa.

Historia ya mji na wakazi

[hariri | hariri chanzo]

Hadi kufikia miaka ya 1950, Batman ilikuwa kijiji kidogo, ila makampuni ya mafuta yalipoingia uchumi wa mji huo ukaanza kukua, na idadi ya makazi ya watu ikaanza kuongezeka.

Wafanyakazi wengi na ofisi nyingi za serikali zipo mjini. Kwa sasa idadi ya watu wasio na kazi katika mji huo inaanza kuonekana kuwa kubwa kuliko hapo awali.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]