Nenda kwa yaliyomo

Klabu za Kiswahili

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
The printable version is no longer supported and may have rendering errors. Please update your browser bookmarks and please use the default browser print function instead.

Klabu za Kiswahili katika shule mbalimbali za sekondari zinaanzishwa kwa malengo mbalimbali.

Yafuatayo ni baadhi ya malengo ya kuanzishwa kwa klabu za lugha ya Kiswahili nchini Tanzania.

*1. Kukuza na kueneza lugha ya Kiswahili ndani na nje ya Tanzania.

*2. Kudumisha umoja na mshikamano wa watumiaji wa lugha ya Kiswahili ndani na nje ya Tanzania.

*3. Kujifunza zaidi juu ya misamiati mipya ya lugha ya Kiswahili baina ya watumiaji (kupitia midahalo na majadiliano).

*4. Kuibua wataalamu hodari wa lugha ya Kiswahili kwa kuzingatia kanuni na taratibu za lugha hiyo (sarufi ya Kiswahili), yaani kimatamshi, kimantiki na kimaana.

*5. Kuandaa wasanifishaji hodari wa lugha ya Kiswahili au kufanya uwiano sawa wa kimatamshi katika lugha hiyo.

*6. Kuibua vipaji mbalimbali vya sanaa, mfano watunzi wa nyimbo, mashairi, ngonjera, hadithi, {simulizi za kusisimua} na majigambo. Kwa lengo la kueneza tamaduni za Kiswahili {Mswahili}.

*7. Kuibua waandaaji hodari wa hotuba za Kiswahili ndani na nje ya nchi ya Tanzania kwa uzingatiaji wa kanuni, taratibu na sheria zote za uandaaji wa hotuba.

*8. Kuandaa wamahiri bora wa lugha ya Kiswahili, yaani wanaoweza kutumia lugha hiyo katika nyanja kuu nne ambazo ni kusoma, kuandika, kusikiliza na kuzungumza kwa ufasaha.

*9. Kuandaa wakalimani hodari wa lugha ya Kiswahili ambao watahamasisha wageni wengi kuwa na shauku ya kujifunza lugha hiyo.

*10. Kuandaa watunzi bora wa kamusi za Kiswahili sanifu.

Changamoto

*1. Uhaba wa fedha zinazotakiwa zitumike katika shughuli mbalimbali za kukiendeleza Kiswahili kama vile kununua vyombo kuhifadhia kazi za kisanaa, mfano vinakilishi.

*2. Uhaba wa wadhamini na wataalamu waliobobea katika lugha ya Kiswahili kwa lengo la kukagua na kukosoa baadhi ya mambo yafanyikayo katika klabu.

*3. Kutokuwepo kwa mahali maalumu pa kufanyia shughuli zote zinazoihusu klabu ya Kiswahili, yaani pahali mahususi pa kuendeshea shughuli zote za klabu.

*4. Kutokuwepo muendelezo wa vipaji vinavyoibuliwa katika klabu, kama vile waandishi wa hotuba, watunzi wa mashairi na waimbaji.

*5. Kukosekana kwa vipaumbele ambavyo vingeweza kuifikisha mbali klabu za Kiswahili. Mfano wa vipaumbele hivyo ni kama vile kuhudhuria katika makongamano mbalimbali ya Kiswahili.

Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Klabu za Kiswahili kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.