Kwa maana tofauti wa jina hili angalia kondoo. Kwa maana tofauti ya Hamali angalia hapa Mpagazi

Nyota kuu za Kondoo (Hamali - Aries)
Kondoo -Hamali jinsi ilivyowazwa na wasanii wa kale

Kondoo (pia: Punda, zamani Hamali, Aries) ni kundinyota ya zodiaki linalojulikana pia kwa jina lake la kimagharibi la Aries[1]. Hamali pia ni jina la kimataifa kwa nyota angavu zaidi kati kundinyota hili.

Nyota za Kondoo huwa haziko pamoja kihalisi lakini zinaonekana tu vile kutoka duniani. Kwa uhalisi kuna umbali mkubwa kati yao, kama ziko mbali au jirani nasi. Kwa hiyo kundinyota "Kondoo" inaonyesha eneo la angani jinsi tunavyoiona kutoka Duniani.

Jina

Kondoo ni tafsiri ya Hamali. Mabaharia Waswahili walijua nyota hizi tangu muda mrefu kwa jina la "Hamali".[2]

Hamali linatokana na Kiarabu حمل ḥamal ambalo linamaanisha "kondoo". Jina hili lilipokelewa na Waarabu kutoka kwa Wagiriki wa Kale waliosema Κριός krios "dume wa kondoo" na hao walipokea tayari (kundinyota)| hii kutoka Babeli. [3] [4]

Katika unajimu wa kisasa katika Afrika ya Mashariki jina "Hamali" limesahauliwa ikiwa kundinyota linatafsiriwa tu "Kondoo".

Mahali pake

Kondoo iko angani kwenye mstari wa Zodiaki kati ya Samaki (pia Hutu, lat. Pisces) na Ng'ombe (pia Tauri, lat. Taurus) .

Magimba ya angani

Kondoo huwa na nyota angavu 3 hasa zilizotumiwa kwa ubaharia tangu zamani.[5] Hizi mara nyingi zinatajwa kama Alpha, Beta na Gamma Arietis [6].

Alpha Arietis inajulikana kimataifa pia kwa jina la "Hamali" kwa sababu majina mengine ya Kiarabu yaliyopokelewa na wanaastronomia wa Ulaya. Ni nyota jitu yenye rangi ya kichungwa na mwangaza unaoonekana wa mag 2.0. Umbali wake na dunia ni mwakanuru 66 na uangavu haĺisi ni −0.1.

Beta Arietis inayoitwa pia Sheratan ina rangi ya buluu-nyeupe na mwangaza unaoonekana wa 2.64 ikiwa umbali wa miakanuru 59 kutoka Dunia.

Jina la
(Bayer)
Namba ya
Flamsteed
Jina
(Ukia)
Mwangaza
unaoonekana
Umbali
(miakanuru)
Aina ya spektra
α 13 Elnath 2,01 0,48 66 K2 III
β 6 Sharatani 2,64 1,33 60 A5 V
c 41 Bharani 3,61 0,16 160 B8 V
γ1,2 5 Mesarthim 3,88 0,8 204 A1
δ Botein 4,35 0,79 168 K2 III

Tanbihi

  1. Uhusika milikishi (en:genitive) ya neno "Aries" katika lugha ya Kilatini ni "Arietis" na hili ni umbo la jina linaloonekana katika majina ya nyota za kundi hili kama vile Alfa Arietis, nk.
  2. ling. Knappert 1993
  3. Edward William Lane , Arabic‐English Lexicon p. 1428, A lamb; alhamal „aries“
  4. Rogers, John H. 1998. "Origins of the Ancient Constellations: I. The Mesopotamian Traditions". Journal of the British Astronomical Association. 108 1: 9–28. Bibcode:1998JBAA..108....9R.
  5. Proper names of stars , blogu ya mwanastronomia Mwingereza Ian Ridpath, iliangaliwa Juni 2017
  6. "Arietis" ni umbo maalum la jina hili la Kilatini "Aries", lenye maana "ya Aries"

Marejeo

  • Richard Hinckley Allen: Star-Names and their Meanings; kwa G. E. Stechert New York, Leipzig, London, Paris 1899, ukurasa 75 ff (online hapa kwenye archive.org)
  • Jan Knappert, 1993: The Swahili Names of Stars, Planets and Constellations; The Indian Ocean Review September 1993 Volume 6 No. 3 September 1993, kurasa 6-7, ISSN 1031-2331


Viungo vya Nje

  Makundinyota ya Zodiaki
Majina ya kisasa yanafuatwa kwa mabano na jina la mabaharia na jina la Kilatini (la kimataifa)
 

Kaa (Saratani – Cancer  )Kondoo (Hamali – Aries  )Mapacha (Jauza – Gemini  )Mashuke (Nadhifa – Virgo  )Mbuzi (Jadi – Capricornus  )MizaniLibra  )Mshale (Kausi – Sagittarius  )Ndoo (Dalu – Aquarius  )Nge (Akarabu – Scorpius  )Ng'ombe (Tauri – Taurus  )Samaki (Hutu – Pisces  )Simba (Asadi – Leo  )