Airbus
Airbus SAS ni kampuni kubwa ya kutengeneza eropleni katika Ulaya na moja ya makampuni makubwa duniani katika fani hii.
Kwa jumla imeajiri watu 50,000 katika nchi mbalimbali na hasa katika viwanda vyake huko Ufaransa, Ujerumani, Uingereza na Hispania.
Tangu mwaka 2001 Airbus imekuwa kampuni inayotengeneza ndege za kusafirisha abiria nyingi duniani. Ni hasa aina mbalimbali kama vile Airbus A300, Airbus A310 au Airbus A320. Tangu mwaka 2007 Airbus A380 ni ndege kubwa kabisa ya kubeba abiria duniani.
Historia
[hariri | hariri chanzo]Kampuni ya Airbus ni tokeo la harakati la kuunganisha makampuni madogo zaidi katika Ulaya kwa shabaha ya kuweza kushindana na makampuni makubwa ya kutengeneza ndege ya Marekani kama vile Boeing na McDonnell Douglas.
Chanzo cha Airbus kilikuwa maungano ya makampuni ya Kijerumani kwa upande mmoja na shirikisho la makampuni ya Kifaransa. Makampuni mengine kutoka Hispania na Uingereza yalijiunga nao na mwanzoni serikali za nchi hizi zilishika asilimia kubwa ya hisa isipokuwa Ujerumani ambako kampuni la Daimler ilishika hisa za taifa hili. Hadi mwaka 2001 Wajerumani na Wafaransa walishika kila asilimia 37.9 za hisa zote, Waingereza asiilimia 20 na Wahispania 4.2.
Baadaye washiriki wote waliungana kwa kuunda kampuni la EADS (European Aeronautic Defence and Space Company) ambayo sasa ni kampuni mama ya Airbus.
Aina za ndege
[hariri | hariri chanzo]Modeli za kiraia za Airbus
[hariri | hariri chanzo]Ndege | Tabia | Abiria kwa kawaida | Idadi juu ya abiria | Imeruka mara ya kwanza | Mwisho wa utengenezaji |
---|---|---|---|---|---|
A300 | injini 2, safu 3 za viti | 228–254 | 361 | 1972-10-28 | 2007-03-27 (jumla ndege 561) |
A310 | injini 2, safu 3 za viti, badiliko la A300 | 187 | 279 | 1982-04-03 | 2007-03-27 (jumla ndege 255) |
A318 | injini 2, safu 2 za viti, ilifupishwa 6.17 m kutoka A320 | 107 | 117 | 2002-01-15 | |
A319 | injini 2, safu 2 za viti, ilifupishwa 3.77 m kutoka A320 | 124 | 156 | 1995-08-25 | |
A320 | injini 2, safu 2 za viti | 150 | 180 | 1987-02-22 | |
A321 | injini 2, safu 2 za viti, ilirefushwa 6.94 m kutoka A320 | 185 | 220 | 1993-03-11 | |
A330 | injini 2, safu 3 za viti | 253–295 | 406–440 | 1992-11-02 | |
A340 | injini 4, safu 3 za viti | 239–380 | 420–440 | 1991-10-25 | 2008-09 (A340-200) 2011-11-10 (modeli zote jumla ndege 375) |
A350 | injini 2, safu 3 za viti | 270–350 | 550 | 2014 (imepangwa) | |
A380 | injini 4, ghorofa 2, safu 3 za viti | 555 | 853 | 2005-04-27 |
Modeli za kijeshi
[hariri | hariri chanzo]Airbus inatengeneza pia modeli mbalimbali za ndege za usafiri wa kijeshi. Sehemu ya hizi zinafanana na modeli za kiraia zilizibadilishwa kwa mahitaji ya kijeshi lanini nyingine zimetengenezwa hasa kwa makusudi ya kijeshi. Airbus haijengi ndege za kutuopa mabomu au ya kushambulia ndege nyingine.