Ja Rule
Ja Rule | |
---|---|
Ja Rule akiwa na Jaid Barrymore mnamo Februari ya mwaka wa 2005 | |
Taarifa za awali | |
Jina la kuzaliwa | Jeffrey Atkins |
Amezaliwa | 29 Februari 1976 Queens, New York City, New York, U.S. |
Kazi yake | Rapper, singer, actor |
Miaka ya kazi | 1994–present |
Studio | Def Jam, The Inc., Mpire Music Group, Fontana Distribution |
Ameshirikiana na | Irv Gotti, DMX, Ashanti, Memphis Bleek, Mary J. Blige |
Jeffrey Atkins (amezaliwa tar. 29 Februari, 1976),[1] anafahamika kwa jina lake la kisanii Ja Rule, ni rapa kutoka nchini Marekani, mwimbaji, na vilevile mwigizaji kutoka mjini Queens, New York.
Alizaliwa mjini Hollis, Queens, alianza kutamba kunako mwaka wa 1999 akiwa na albamu ya Venni Vetti Vecci na kibao chake kikali cha "Holla Holla". Kuanzia 1999 hadi 2005, Ja Rule amekuwa na vibao kadhaa vilivyoingia kwenye 20 bora ya chati za Billboard Hot 100, ikiwa ni pamoja na "Between Me and You" akishirikiana na Christina Milian, "I'm Real (Murder Remix)" na Ain't It Funny akiwa na Jennifer Lopez, ambazo zote zilitingisha katika chati za US Billboard Hot 100, kibao namba 1 kilichobahatika kuchaguliwa katika Tuzo za Grammy, "Always on Time" akiwa na Ashanti, "Mesmerize" nacho pia alikuwa na Ashanti, na "Wonderful" akiwa na R. Kelly na Ashanti.
Wakati wa miaka ya 2000, Ja Rule aliingia mkataba na The Inc. Records, ambayo awali ilikuwa ikitambulika kama Murder Inc. na ilikuwa ikiongozwa na Irv Gotti. Kutokana na vibao vyake na washirika wake, Ja Rule amepokea chaguzi nne za Grammy, na albamu zake sita zimeiingia katika kumi bora, mbili katika hizo ni Rule 3:36 (2000) na Pain Is Love (2001), imegonga vyema katika chati za US Billboard 200. Pia anafahamika sana katika jamii kwa kuwa na mgogoro na baadhi ya marapa wengine kama vile (hasa 50 Cent na Eminem).
Maisha ya awali
[hariri | hariri chanzo]Kazi ya muziki
[hariri | hariri chanzo]Diskografia
[hariri | hariri chanzo]- Albamu za Studio
- 1999: Venni Vetti Vecci
- 2000: Rule 3:36
- 2001: Pain Is Love
- 2002: The Last Temptation
- 2003: Blood in My Eye
- Albamu zingine
- 2004: R.U.L.E.
- 2012: Pain Is Love 2[2]
- Albamu huru
- 2009: The Mirror
- Albamu za kompilesheni
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Birchmeier, Jason (2007). "AllMusic Biography". allmusic. Iliwekwa mnamo Desemba 13, 2010.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Kuperstein, Slava (2011-03-19). "DX News Bits: Lil Wayne Signs Porcelain Black, Ja Rule Plans 2 Albums In 1 Day, Rev. Run Signs Watch Deal | Get The Latest Hip Hop News, Rap News & Hip Hop Album Sales". HipHop DX. Iliwekwa mnamo 2012-12-13.
Viungo vya Nje
[hariri | hariri chanzo]- Official website
- The Inc. artist website (archived)
- Ja Rule katika MySpace
- Kigezo:MTV artist
- Ja Rule at the Internet Movie Database