Nenda kwa yaliyomo

Karagosi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Maonyesho ya mchezo wa karagosi za mkono (mchezaji haonekani yuko nyuma ya jukwaa
Karagosi nyuzi

Karagosi (kutoka Kituruki karagöz = jicho cheusi) ni mwanaserere au mdoli anayetumiwa kwa ajili ya igizo mbele ya watazamaji. Nafasi ya karagosi ni ile ya mwigizaji katika tamthiliya. Sauti yake ni ya binadamu aliye kando la jukwaa au anayejificha nyuma yake.

Kuna aina mbalimbali za karagosi kwa mfano:

  • karagosi ya mkono inayowekwa juu ya mkono; huwa na kichwa kilichochongwa (ubao au ufinyanzi) na nguo; mkono wa mwigizaji haionekani ndani ya nguo na kidole cha shahada kinaingia katika nafasi ndani ya kichwa; kidole gumba na kidole cha kati .
  • karagosi nyuzi (marioneti); huwa na viungo na vifundo vinavyotawaliwa na mchezaji kwa njia ya kuvuta nyuzi zinazounganishwa na kila kiungo.

Karagöz ya Kituruki

[hariri | hariri chanzo]

Jina la karagosi limetokana na jukumu katika maigizo ya tamthiliya ya madoli ya Uturuki. Kimapokeo aina hii ya tamthiliya huwa na jukumu mbili za Karagöz ambaye ni mtu maskini bila elimu na Hacivat ambaye ni mtu wa tabaka ya wastani au pia ya juu. Aina hii ya tamthiliya inatumia picha za watu zinazosukumwa kwa mafimbo nyuma ya kiwambo kilichoangazwa kwa taa kutoka nyuma; hivyo kivuli cha rangi kinaonekana. Tamthiliya ya Karagöz ilikuwa maonyesho yaliyopendwa sana na watu yaliendelea hata baada kujitokeza kwa filamu katika karne ya 20 lakini tangu usambazaji wa televisheni na video zimepungua.