Kipanya manyoya-mororo
Mandhari
Kipanya manyoya-mororo | ||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Kipanya manyoya-mororo wa Dalton nchini Mauritania (Praomys daltoni)
| ||||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||
| ||||||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||||||
Spishi 8:
|
Vipanya manyoya-mororo ni wanyama wagugunaji wa jenasi Praomys katika nusufamilia Murinae ya familia Muridae wanaotokea katika misitu minyevu ya Afrika kusini kwa Sahara.
Maelezo
[hariri | hariri chanzo]Panya hawa wana manyoya mororo ambayo yanaweza mafupi au marefu. Pua ni ndefu na masikio ni makubwa na ya mviringo. Urefu wa mwili ni mm 90-140, urefu wa mkia ni mm 110-170 na uzito ni g 12-70. Rangi yao ni njano, hudhurungi, kahawianyekundu au kijivu mgongoni na nyeupe au njano tumboni.
Wanapatikana katika misitu minyevu na hukiakia usiku. Hutumia sehemu ya wakati wao katika miti na hujenga viota kwa majani pia mitini au ardhini, pengine katika vishimo. Hula matunda, mbegu na sehemu kijani za mimea, na wadudu pia.
Spishi
[hariri | hariri chanzo]- Praomys coetzeei (Coetzee's soft-furred mouse)
- Praomys daltoni (Dalton's mouse)
- Praomys degraaffi, Kipanya Manyoya-mororo wa De Graaff (De Graaff's soft-furred mouse) – Burundi, Rwanda, Uganda
- Praomys delectorum, Kipanya Manyoya-mororo Taanusi (Delectable soft-furred mouse) – Kenya, Tanzania
- Praomys derooi (Deroo's mouse)
- Praomys hartwigi (Hartwig's soft-furred mouse)
- Praomys jacksoni, Kipanya Manyoya-mororo wa Jackson (Jackson's soft-furred mouse) – Burundi, Kenya, Rwanda, Tanzania, Uganda
- Praomys lukolelae (Lukolela swamp mouse)
- Praomys minor (Least soft-furred mouse)
- Praomys misonnei, Kipanya Manyoya-mororo wa Misonne (Misonne's soft-furred mouse) – Kenya, Uganda
- Praomys morio (Cameroon soft-furred mouse)
- Praomys mutoni (Muton's soft-furred mouse)
- Praomys obscurus (Gotel Mountain soft-furred mouse)
- Praomys petteri (Petter's soft-furred mouse)
- Praomys rostratus (Forest soft-furred mouse)
- Praomys tullbergi (Tullberg's soft-furred mouse)
- Praomys verschureni (Verschuren's swamp mouse)