Kisiwa cha Norfolk
| |||||
Kaulimbiu ya taifa: "Inasmuch" | |||||
Wimbo wa taifa: Advance Australia Fair (Sogea mbele Australia nzuri) | |||||
Mji mkuu | Kingston | ||||
Mji mkubwa nchini | Burnt Pine | ||||
Lugha rasmi | Kiingereza | ||||
Serikali Mkuu wa Dola
Afisa Mtendaji Waziri wa kwanza |
Eneo la ng'ambo la Australia Elizabeth II wa Uingereza Grant Tambling David Buffett | ||||
Madaraka ya kujitawala Sheria ya Norfolk |
1979 | ||||
Eneo - Jumla - Maji (%) |
34.6 km² (ya 226) 0 | ||||
Idadi ya watu - 2004 kadirio - Msongamano wa watu |
1,841 (ya 232) 53.2/km² (ya 191) | ||||
Fedha | Dollar ya Australia (AUD )
| ||||
Saa za eneo - Kiangazi (DST) |
NFT (Norfolk Island Time) (UTC+11:30) (UTC) | ||||
Intaneti TLD | .nf | ||||
Kodi ya simu | +6723
- |
Kisiwa cha Norfolk ni eneo la ng'ambo la Australia katika Pasifiki ya Kusini kati ya Australia, New Zealand na Kaledonia Mpya.
Jiografia
[hariri | hariri chanzo]Kisiwa kipo takriban 1500 km upande wa mashariki ya Australia. Pamoja na visiwa vidogo jirani vya Nepean na Phillip ni ya asili ya kivolkeno hivyo kuna ardhi yenye rutuba kwa ajili ya kilimo.
Historia
[hariri | hariri chanzo]Kisiwa kiliwahi kukaliwa na Wapolynesia jinsi inavyoonekana kwa mabaki ya kijiji kilichogunduliwa na waakiolojia na kuwepo kwa panja na ndizi ambazo zilisambazwa na Wapolynesia kwenye visiwa vya Pasifiki.
Lakini wakati wa kufika kwa nahodha Mwingereza James Cook mwaka 1774 kisiwa kilikuwa bila watu. Cook alikipa jina la Norfolk kwa heshima ya kabaila Mwingereza fulani aliyeitwa hivyo.
Kuanzia 1788 kisiwa kikakaliwa na wafungwa kutoka magereza ya Uingereza na Australia. Lakini majaribio haya yameachwa tena na makambi ya wafungwa kuhamishwa penginepo.
Mwaka 1856 mababu wa kwanza wa wakazi wa leo walifika kutoka Pitcairn. Idadi ya wajukuu wa waasi wa Bounty ilikuwa imeongezeka mno kwa kisiwa kidogo na serikali ya Uingereza iliwahamisha watu 194 kwenda Norfolk.
Leo hii theluthi moja ya wakazi wa Norfolk ni wa asili ya Pitcairn. Wengine wamekuja kutoka Australia au kutoka Polynesia.
Makala hii kuhusu eneo fulani bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu eneo hilo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Je, unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.
|
Nchi_na maeneo ya Australia na Pasifiki |
Australia | Fiji | Guam | Hawaii | Kaledonia Mpya | Kiribati | Kisiwa cha Pasaka | Mikronesia | Nauru | Nyuzilandi | Niue | Pitcairn | Polinesia ya Kifaransa | Palau | Papua Guinea Mpya | Samoa | Samoa ya Marekani | Visiwa vya Cook | Visiwa vya Mariana ya Kaskazini | Visiwa vya Marshall | Visiwa vya Solomon | Tonga | Tuvalu | Vanuatu | Wallis na Futuna |