Kobalti
Kobalti | |
---|---|
Kobalti
| |
Jina la Elementi | Kobalti |
Alama | Co |
Namba atomia | 27 |
Mfululizo safu | Metali |
Uzani atomia | 58.933 |
Valensi | 2, 8, 15, 2 |
Densiti | 8.90 g/cm³ |
Ugumu (Mohs) | {{{ugumu}}} |
Kiwango cha kuyeyuka | 1768 K (1495 °C) |
Kiwango cha kuchemka | 3200 K (2927 °C) |
Asilimia za ganda la dunia | 4.7 % |
Hali maada | mango |
Kobalti (kutoka Kiingereza cobalt inayotoka Kijerumani kobalt) ni elementi na metali haba duniani. Kikemia ni elementi mpito yenye kifupi cha Co na namba atomia 27 katika mfumo radidia yenye uzani atomia 58.933.
Kobalti hupatikana mara chache kama metali tupu lakini zaidi ndani ya mitapo hasa za nikeli na shaba.
Tangu kale kampaundi zake hutumiwa kwa rangi na wino mbalimbali, hasa za buluu, kijani na njano. Kampaundi ya CoAl2O4 inatumiwa kutengeneza kioo cha buluu.
Katika karne ya 20 matumizi yalienea katika uzalishaji wa feleji, aloi yake inaongeza ugumu wa feleji.
Tangu kupatikana kwa simu za mkononi na magari ya umeme kobalti imekuwa muhimu sana kwa uzalishaji wa beteri. Hii ilisababisha mlipuko wa soko la kobalti na uchimbaji wake. Mwaka 2016 takriban asilimia 60 za mahitaji yote yalichimmbwa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo[1].
Land | 2006[2] | 2013[3] | 2016[4] |
---|---|---|---|
Australia | 6000 | 6400 | 5100 |
Brazil | 1000 | 3000 | 5800 |
China | 1400 | 7200 | 7700 |
JD Kongo | 22000 | 54000 | 66000 |
Kanada | 5600 | 6920 | 7300 |
Kuba | 4000 | 4200 | 4200 |
Moroko | 1500 | 1700 | |
Kaledonia Mpya | 1100 | 3190 | 3300 |
Ufilipino | 3000 | 3500 | |
Urusi | 5100 | 6300 | 6200 |
Zambia | 8600 | 5200 | 4600 |
Afrika Kusini | 3000 | 3000 | |
nchi nyingine za Dunia | 1200 | 8000 | 8300 |
Jumla | 57.500 | 110.000 | 123.000 |
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ The hottest thing in the markets right now is an obscure metal mined in DR Congo, tovuti ya Quartz.com ya April 27, 2017, iliangaliwa Januari 2018
- ↑ Cobalt 2007 kwa USGS Mineral Resources.
- ↑ Cobalt 2014 kwa USGS Mineral Resources
- ↑ Cobalt 2016 kwa USGS Mineral Resources
Makala hii kuhusu mambo ya kemia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Kobalti kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |