Nenda kwa yaliyomo

Kronos

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kronos akishika mundu aliyotumia kumhatinisha babake Uranos

Kronos alikuwa mungu mmojawapo katika dini ya Ugiriki ya Kale aliyekuwa mkuu wa miungu wa nasaba ya Watitani na mtawala wa ulimwengu katika kipindi kabla ya Zeus na miungu ya Olimpi.

Kadiri ya hadithi, Kronos alikuwa mwana wa mwisho wa Uranos na Gaia na kwa kufuata ushauri wa mama yake Gaia alimhatinisha baba yake Uranos kwa mundu. Baadaye aliogopa ya kwamba mmoja wa watoto wake angempindua pia, hivyo alimeza watoto wake aliyezaa na dada yake na mke Rhea. Mwishoni Rhea alifaulu kumficha mwana wake wa mwisho Zeus maana wakati Kronos alitaka kummeza Zeus alipewa jiwe lililoviringishwa katika vitambaa vya mtoto na kuimeza.

Zeus alimpindua baba yake baadaye akamfunga na kumfukuza mbinguni akamtuma kutawala juu ya kisiwa cha heri.

Baadaye Waroma wa Kale walimtazama kama jina tofauti la mungu wao Saturnus wakaendelea kusimulia hadithi za Kronos juu yake.