Malko
Malko ni mwanamume wa karne ya 1 ambaye alikuwa mtumishi wa kuhani mkuu wa Israeli.
Ni maarufu kwa sababu anatajwa katika Injili kama mmojawapo kati ya watu waliokwenda katika bustani ya Gethsemane usiku wa kuamkia Ijumaa Kuu ili kumkamata Yesu Kristo.
Alipomfikia tu, Mtume Petro, akiwa na upanga, alimkata sikio la kulia katika juhudi zake za kumuokoa Yesu. Tukio hilo linapatikana katika Injili zote nne[1]: Math 26:51; Mk 14:47; Lk 22:50-51 na Yoh 18:10-11. Kumbe jina la mtu aliyepigwa linatajwa na Yohane tu.
Upande wake, Luka peke yake anasimulia kuwa Yesu alirudisha sikio lililokatwa mahali pake: ndio muujiza wake wa mwisho, nao ulitendwa kwa ajili ya adui kama utekelezaji wa fundisho lake la kwamba ni lazima kuwatendea mema wanaotutenda mabaya.
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- "Malchus". Catholic Encyclopedia. New York: Robert Appleton Company. 1913.
Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Malko kama habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |