Mr. & Mrs. Smith
Mr. & Mrs. Smith | |
---|---|
Imeongozwa na | Doug Liman |
Imetayarishwa na | Akiva Goldsman Arnon Milchan |
Imetungwa na | Simon Kinberg |
Nyota | Brad Pitt, Angelina Jolie, Vince Vaughn Kerry Washington Adam Brody |
Muziki na | John Powell |
Imehaririwa na | Michael Tronick |
Imesambazwa na | 20th Century Fox |
Imetolewa tar. | Juni 10, 2005 |
Ina muda wa dk. | Theatrical cut 120 minutes Unrated cut 123 minutes |
Nchi | Marekani |
Lugha | Kiingereza |
Bajeti ya filamu | $110 million |
Mapato yote ya filamu | $478,336,279 |
Mr. & Mrs. Smith ni filamu ya 2005 yenye kupigana na kuchekesha iliyotayarishwa na Doug Liman na kuandikwa na Simon Kinberg. Muziki wake ulitungwa na John Powell. Wahusika wa filamu hii ni Angelina Jolie na Brad Pitt.
Hadithi
[hariri | hariri chanzo]Filamu hii inaanza pindi John (Brad Pitt) na Jane Smith (Angelina Jolie) wanajibu maswali yanayohusu ndoa yao. Maharusi hawa waneoana kwa muda wa "miaka tano au sita", lakini ndoa yao inapata pandashuka nyingi hadi wawili hawa hawajui ni lini mwisho walifanya kitendo cha ndoa. Wanaeleza jinsi walivyokutana kwa mara ya kwanza mjini Bogotá, Colombia baada ya kufukuzwa na askari. Walipendana baada ya hapo na kuoana.
Wote hawa ni wauaji wanaofanya kazi makampuni tofauti, na wote wanaficha siri hii. Jane na John wanatumwa kumuuwa Benjamin Danz. Baada ya kugunduana, wapenzi hawa wanapigana na kutaka kuuana. Baada ya kupigana kwa muda mrefu, Jane anamshikia bunduki mumewe lakini anashindwa kkupiga risasi kwa ajili ya mahaba aliyonayo. Hivyo basi, wote wanakumbatiana na kuanza upya mapenzi yao.
Kwa bahati mbaya, rafiki yake John aitwaye Addie anatumwa kuwaua John na Jane kisha atapewa $400,000. Hivyo basi, familia ya Smiths inaamua kupigana kwa pamoja ili kuokoa ndoa yao. Mwishowe, Jane na John wanashirikiana vizuri kuwaua kundi la wanajeshi waliotumwa kuwamaliza.
Filamu hii inamalizika pindi wawili hawa wanaenda kwa mkutano kuhusu ndoa yao, ambapo wanasema jinsi walivyo na raha wakiwa pamoja.
Wahusika
[hariri | hariri chanzo]- Brad Pitt - John Smith
- Angelina Jolie - Jane Smith
- Vince Vaughn- Eddie
- Kerry Washington - Jasmine
- Adam Brody - Benjamin "The Tank" Danz
- Keith David - Father
- Chris Weitz - Martin Coleman
- Rachael Huntley - Suzy Coleman
- Michelle Monaghan- Gwen
- Benton Jennings - Maitre'D
- Stephanie March - Julie
- Jennifer Morrison - Jade
- Theresa Barrera - Janet
- Perrey Reeves - Jessie
- Melanie Tolbert - Jamie
- Angela Bassett - sauti ya meneja wa Mr. Smith
- William Fichtner - Dkt Waxleg
Mapokezi
[hariri | hariri chanzo]Hadi 26 Oktoba 2009, filamu hii imepata mauzo ya $478,336,279 kote duniani..[1]
Wimbo
[hariri | hariri chanzo]Albamu mbili zilitolewa kutoka kwa filamu hii: moja ikiwa na wimbo uliotungwa na John Powell na nyingine ikiwa na nyimbo zilizotumika kwenye filamu hii. Albamu hizi zilitolewa tarehe tofauti: 28 Juni 2005 na 7 Juni 2005.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Mr. And Mrs. Smith". The Numbers. Nash Information Services, LLC. 26 Oktoba 2009. Iliwekwa mnamo 2010-01-10.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Mr. & Mrs. Smith at the Internet Movie Database
- Mr. & Mrs. Smith katika Sanduku la Ofisi la Mojo
- Mr. & Mrs. Smith katika Rotten Tomatoes
- Mr. & Mrs. Smith katika Metacritic