Oyani
Mandhari
Oyani | ||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Oyani wa Afrika ya Kati (Poiana richardsonii)
| ||||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||
| ||||||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||||||
Spishi 2:
|
Oyani (kutoka Kiing.: oyan[1][2]) ni wanyama mbua wadogo wa jenasi Poiana katika familia Viverridae. Wanafanana sana na linisang'i wa Asia (jenasi Prionodon) lakini wanyama hawa wana mnasaba zaidi na paka (Felidae) na wamo katika familia yao binafsi Prionodontidae[3]. Oyani wana mnasaba na kanu. Mfanano na linisang'i ni mfano wa mageuko ya ukaribiano.
Oyani ni wadogo (mwili wa sm 30 na mkia wa zaidi ya sm 30) lakini wembamba wenye miguu mifupi. Rangi yao ni aina ya njano na wana mabaka meusi (madoa, milia) na mkia una zingo nyeusi. Huishi mitini na hukiakia usiku. Hula vitu vyingu kama wanyama na ndege wadogo, wadudu, matunda, koko na machipukizi ya mimea.
Spishi
[hariri | hariri chanzo]- Poiana leightoni, Oyani Magharibi (Leighton's Linsang)
- Poiana richardsonii, Oyani wa Afrika ya Kati (African Linsang)
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Wozencraft, W. Christopher (2005). "Order Carnivora (pp. 532-628)". In Wilson, Don E., and Reeder, DeeAnn M., eds. Mammal Species of the World: A Taxonomic and Geographic Reference (3rd ed.). Baltimore: Johns Hopkins University Press, 2 vols. (2142 pp.). ISBN 978-0-8018-8221-0. OCLC 62265494
- ↑ Don E. Wilson , Russell A. Mittermeier (editors): Handbook of the Mammals of the World. Lynx Editions, Barcelona, 2009. ISBN 978-84-96553-49-1
- ↑ "Nakala iliyohifadhiwa" (PDF). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2007-01-25. Iliwekwa mnamo 2011-11-21.