Sergio Busquets
Sergio Busquets Burgos (alizaliwa 16 Julai 1988) ni mchezaji wa soka wa Hispania ambaye anacheza kama kiungo mkabaji kwenye timu ya Barcelona F.C. na timu ya taifa ya Hispania.
Busquets aliwasili katika timu ya kwanza Barcelona Julai 2006, na hatimaye alichiza kwa muda mfupi,Alipofika tu Barcelona aliitwa akacheze kombe la dunia katika timu yake ya taifa ya Hispania.
Busquets iliisaidia Hispania kushinda Kombe la Dunia 2010 na mashindano ya Euro 2012. Pia aliwakilisha taifa kwenye makombe mawili ya Dunia na Euro 2016.
Mtindo wa kucheza
[hariri | hariri chanzo]Busquets kawaida hutumiwa kama kiungo wa kati au kushoto, ingawa pia anaweza kucheza kama mlinzi wa kati.Busquets ni mchezaji anayefanya kazi kwa bidii,pia ni mchezaji ambaye anajihamini,ana akili ya mchezo na mwenye uwezo wa kuusoma mchezo jinsi ulivyo.
Kwa sababu ya maono yake,udhibiti wa mpira, uwezo wa kimwili, ujuzi wa kiufundi na uwezo wa kupitisha pasi kwenye watu wengi,Busquets pamoja na wachezaji wenzake wa sasa na wa zamani , kama vile Iniesta, Xavi na Ivan Rakitić,wamefanya jukumu muhimu sana katika timu yao ya FC Barcelona.
Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Sergio Busquets kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |