Nenda kwa yaliyomo

Stempu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Penny Black, stempu ya kwanza duniani.
Sehemu muhimu za stempu:
1. Picha
2. Matundu
3. Thamani
4. Jina la nchi

Stempu (kutoka neno la Kiingereza "stamp", yaani "kilichochapwa") ya posta ni kijipande cha karatasi ambacho kinauzwa ili kubandikwa juu ya barua au kifurushi kama thibitisho la malipo ya gharama ya usafirishaji wake.

Pengine uzuri wake unafanya watu wazikusanye badala ya kuzituma au baada ya kutumiwa.

Stempu ya kwanza ilitolewa Uingereza tarehe 1 Mei 1840. Kutoka huko stempu zimeenea duniani kote.