Tunguhina
Mandhari
Tunguhina | ||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||
| ||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||
Spishi 2:
|
Tunguhina ni ndege wadogo wa jenasi Uraeginthus katika familia ya Estrildidae ambao wana rangi kahawianyekundu na viraka buluu au zambarau. Kuna spishi tatu zingine kwa jenasi hii ambazo zinaitwa vitenduli na zina rangi buluu. Wataalamu wengine wanaweka spishi mbili za tunguhina ndani ya jenasi Granatina. Spishi hizi zinatokea Afrika chini ya Sahara tu. Tunguhina ni ndege waoga, lakini kwa bustani ya hoteli na nyumba wanazoea watu. Tago lao hutengenezwa na manyasi ndani ya magugu; limefunikika juu na lina mwingilio kando.
Spishi
[hariri | hariri chanzo]- Uraeginthus granatinus, Tunguhina Kusi (Common Grenadier or Violet-eared Waxbill)
- Uraeginthus ianthinogaster, Tunguhina Kaskazi (Purple Grenadier)
Picha
[hariri | hariri chanzo]-
Tunguhina kusi
-
Tunguhina kaskazi