Gabon
Gabon, kirasmi Jamhuri ya Gabon, ni nchi huru ya Afrika ya Magharibi ya kati.
Jamhuri ya Gabon | |
---|---|
République Gabonaise (Kifaransa) | |
Kaulimbiu ya taifa: Union, Travail, Justice (Kifaransa) "Umoja, Kazi, Haki" | |
Wimbo wa taifa: La Concorde (Kifaransa) "Mapatano" | |
Mahali pa Gabon | |
Ramani ya Gabon | |
Mji mkuu na mkubwa nchini | Libreville |
Lugha rasmi | Kifaransa |
Makabila | Kupita makabila 40 |
Serikali | Jamhuri yenye baraza la majeshi |
• Kaimu Rais | Brice Oligui Nguema |
Eneo | |
• Eneo la jumla | km2 267 668 |
Idadi ya watu | |
• Kadirio la 2023 | 2 397 368 |
Pato la taifa | Kadirio la 2023 |
• Jumla | USD bilioni 19.319 |
• Kwa kila mtu | USD 8 831 |
Pato halisi la taifa | Kadirio la 2023 |
• Jumla | USD bilioni 41.922 |
• Kwa kila mtu | USD 19 165 |
Maendeleo (2021) | 0.706 - juu |
Sarafu | Faranga ya CFA |
Majira ya saa | UTC+1 (Afrika ya Magharibi) |
Msimbo wa simu | +241 |
Msimbo wa ISO 3166 | GA |
Jina la kikoa | .ga |
Imepakana na Guinea ya Ikweta, Kamerun, Jamhuri ya Kongo na Ghuba ya Guinea.
Nchi hii ina umma mdogo, madini na mali kwa wingi, na wafanyabiashara kutoka nchi za kigeni wameweza kufanya Gabon iwe nchi yenye maendeleo makubwa.
Jiografia
haririMaeneo ya utawala
haririGabon imegawiwa katika mikoa 9 nayo ina jumla ya wilaya (départements) 37.
Mikoa ni:
Historia
haririJamhuri ya Gabon, tangu kupata uhuru kutoka Ufaransa tarehe 17 Agosti 1960, imeongozwa na Rais watatu, Léon M'ba, El Hadj Omar Bongo ambaye amekuwa kiongozi kutoka mwaka wa 1967 hadi kifo chake (2009: ndiye aliyekuwa kiongozi barani Afrika aliyeshikilia uongozi kwa muda mrefu zaidi), halafu mwanae Ali aliyepinduliwa na wanajeshi tarehe 30 Agosti 2023.
Siasa
haririMwaka wa 1990 Gabon ilianza demokrasia ya vyama vingi na katiba ya kidemokrasia ili ruhusu ukweli wa uchaguzi na uwajibikaji wa idara za serikali, lakini hali iliendelea kuwa karibu ileile.
Uchumi
haririGabon ni nchi yenye neema sana kuliko nchi jirani. Uchumi wake, hasa chumo cha umma, ni mara nne ya nchi za Afrika kusini kwa Sahara. Hii hasa ni kwa sababu ya uzalishaji wa mafuta ambao umeleta utajiri na mali, lakini usambazaji wa mali hii ya mafuta bado umedhoofika.
Gabon ilikuwa mwanachama wa Muungano wa Nchi Zinazouza Mafuta (OPEC) kutoka mwaka wa 1975 mbaka 1995.
Mwaka 1990, udhaifu wa pesa CFA frank uliacha Gabon katika shida ya kulipa deni za kimataifa; Ufaransa na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) wameipa Gabon mkopo na usaidizi kwa uelewano kwamba Gabon itageuza uchumi wake barabara.
Watu
haririYasemekana mambo ya mazingira yalifanya umma wa Gabon kutopanda kwa sensa kati ya miaka 1900 na 1940.
Ni nchi ambayo ina umma mdogo zaidi katika Afrika bara, na upungufu wa wafanyakazi ni mojawapo ya mambo yanayofanya hasa uchumi kutovuma zaidi.
Umma hasa kwa ujumla ni kama watu milioni 2.4.
Gabon hasa ina makabila zaidi ya 40 ambayo yana utamaduni na lugha tofauti lakini karibu wote (95%) ni wa jamii ya Bantu. Wafang ndio kabila kubwa zaidi nchini Gabon, wengine ni Wamyene, Wabandjabi, Waeshira, Wabapounou na Waokande.
Lugha ya Kifaransa ndiyo lugha rasmi ya taifa ambayo hutumika kwa mawasiliano (wakazi wanaoimudu ni 80%). Wafaransa 10,000 wanaishi Gabon, na Ufaransa unaathiri mambo ya kigeni, utamaduni na biashara nchini Gabon.
Upande wa dini, imekadiriwa kwamba 75.6% za wakazi ni Wakristo (hasa Wakatoliki), 12.2% ni Waislamu (hasa wageni), na 5.7% wanafuata dini asilia za Kiafrika (Bwiti).
Utamaduni
haririTazama pia
hariri- Mawasiliano nchini Gabon
- Mambo ya kigeni ya Gabon
- Orodha ya kampuni za Gabon
- Jeshi la Gabon
- Historia ya Gabon
- Uchukuzi nchini Gabon
- Orodha ya nchi kufuatana na wakazi
- Orodha ya nchi za Afrika kulingana na idadi ya watu
- Orodha ya nchi za Afrika kulingana na msongamano wa watu
- Orodha ya nchi za Afrika kulingana na pato la taifa
- Demografia ya Afrika
Marejeo
hariri- David E. Gardinier and Douglas A. Yates, Historia elekezo ya Gabon, tolezi ya 3. (The Scarecrow Press, Inc., 2006)
- David E. Gardinier, Kamusi ya Historia ya Gabon, tolezi ya 2. (The Scarecrow Press, Inc., 1994) – kazi inayohusu maelezo biografia ya vifaa 1,453
- James F. Barnes, Gabon: Beyond the Colonial Legacy (Boulder: Westview, 1992)
Viungo vya nje
haririSerikali
hariri- Le Gabon : makala rasmi ya Jamhuri ya Gabon Archived 29 Machi 2007 at the Wayback Machine.
- Assemblée nationale du Gabon makala rasmi.
- Gabonese Embassy in London Archived 22 Septemba 2019 at the Wayback Machine. arithio za serikali
- Le Sénat de la République Gabonaise makala rasmi (kwa kifaransa)
Habari
hariri- AllAfrica.com - Gabon viungo via taarifa ya habari
Uchambuzi
hariri- BBC News Country Profile - Gabon
- Kitabu cha wa dadisi wa Amerika - Gabon Archived 2 Mei 2006 at the Wayback Machine.
Koo na makabila
hariri- Baka watu wafupi wa Kamerun na Gabon Utamaduni na wakazi wa kwanza Gabon
Maelekezo
hariri- Open Directory Project - Gabon Archived 24 Aprili 2006 at the Wayback Machine. maelekezo
- Chuo kikuu cha Stanford – Afrika kusini mwa sahara: Gabon maelekezo
- Chuo kikuu cha Pennsylvania – Ustadi wa-Afrika: Gabon maelekezo
- Yahoo! - Gabon Archived 28 Aprili 2006 at the Wayback Machine. directory category
Utalii
hariri
Nchi za Afrika | |
---|---|
Afrika ya Kati (Jamhuri ya) | Afrika Kusini | Algeria | Angola | Benin | Botswana | Burkina Faso | Burundi | Cabo Verde | Chad | Cote d'Ivoire | Eritrea | Eswatini | Ethiopia | Gabon | Gambia | Ghana | Guinea | Guinea Bisau | Guinea ya Ikweta | Jibuti | Kamerun | Kenya | Komori | Kongo (Jamhuri ya) | Kongo (Jamhuri ya Kidemokrasia ya) | Lesotho | Liberia | Libya | Madagaska | Malawi | Mali | Misri | Morisi (Visiwa vya) | Mauritania | Moroko | Msumbiji | Namibia | Niger | Nigeria | Rwanda | Sahara ya Magharibi | Sao Tome na Principe | Senegal | Shelisheli | Sierra Leone | Somalia | Sudan | Sudan Kusini | Tanzania | Togo | Tunisia | Uganda | Zambia | Zimbabwe | |
Maeneo ya Afrika ambayo ni sehemu za nchi nje ya Afrika | |
Hispania: Kanari · Ceuta · Melilla | Italia: Pantelleria · Pelagie | Ufaransa: Mayotte · Réunion | Uingereza: · St. Helena · Diego Garcia | Ureno: Madeira |
Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Gabon kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |