Nenda kwa yaliyomo

Membe

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
The printable version is no longer supported and may have rendering errors. Please update your browser bookmarks and please use the default browser print function instead.

Kwa matumizi mengine za jina hili angalia Membe (maana)

Membe
Membe sululu
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Aves (Ndege)
Oda: Charadriiformes (Ndege kama vitwitwi)
Familia: Scolopacidae (Ndege walio na mnasaba na sululu)
Jenasi: Bartramia Lesson, 1831

Numenius Brisson, 1760

Spishi: Angalia katiba

Membe ni ndege wa jenasi Numenius katika familia ya Scolopacidae. Bartramia longicauda ana mnasaba sana na membe. Ndege hawa ni wakubwa kabisa katika familia hii. Wana miguu mirefu na mdomo mrefu unaopingwa chini (isipokuwa Bartramia). Wana rangi kahawia na madoa na michirizi nyeupe mwaka mzima. Hutafuta chakula kwa matope wakiingiza mdomo mrefu wao, na hula nyungunyungu, daa, wadudu na gegereka. Hutaga mayai 3-6 ardhini kwa manyasi.

Spishi za Afrika

Spishi za mabara mengine

Picha