Nenda kwa yaliyomo

Petrus Plancius

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
The printable version is no longer supported and may have rendering errors. Please update your browser bookmarks and please use the default browser print function instead.
Petrus Plancius. J. Buys/Rein. Vinkeles (1791).

Petrus Plancius (155215 Mei 1622) alikuwa mwanatheolojia, mchungaji wa Kanisa la Kireformed, mwanaastronomia na mchoraji wa ramani kutoka Flandria aliyeishi miaka mingi huko Uholanzi.

Tangu mwaka 1589 alianza kuchora ramani za nyota ambako aliingiza mara ya kwanza kundinyota nyingi za nusutufe ya kusini zilizoanza kujulikana Ulaya baada ya mabaharia wa Ulaya kuzunguka dunia yote. Hapo alichora mara ya kwanza Salibu, Pembetatu ya Kusini na Mawingu ya Magellan.

Mwaka 1595 Plancius alimwomba nahodha Mholanzi Pieter Dirkszoon Keyser kukusanya vipimo vya nyota za kusini zisizopimwa bado, akazipanga katika makundinyota mapya 12 na hizi zilikuwa Nzi (Musca), Ndege wa Peponi (Apus), Kinyonga (Chamaeleon), Panji (Dorado), Kuruki (Grus), Nyoka Maji (Hydrus), Mhindi (Indus), Tausi (Pavo), Zoraki (Phoenix), Pembetatu ya Kusini (Triangulum Australe), Tukani (Tucana) na Panzimaji (Volans) akaziweka zote katika globus yake ya nyota.

Mwaka 1612 aliongeza makundinyota mawili kwenye nusutufe ya kaskazini akipanga humo nyota ambazo hazikuwa bado sehemu ya makundinyota yalizojulikana. Nayo ni Twiga (Camelopardalis) karibu na ncha ya anga ya kaskazini na Munukero (Monoceros) kwenye ikweta ya anga.

Baadaye makundinyota yake yalipokewa vile na Johann Bayer katika orodha yake na kutumiwa hadi leo katika orodha ya Umoja wa Kimataifa wa Astronomia.

Ramani

Marejeo


Viungo vya Nje

Makala hii kuhusu mwanasayansi fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Petrus Plancius kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.