26 Juni
Mandhari
Mei - Juni - Jul | ||||||
1 | 2 | 3 | 4 | 5 | 6 | 7 |
8 | 9 | 10 | 11 | 12 | 13 | 14 |
15 | 16 | 17 | 18 | 19 | 20 | 21 |
22 | 23 | 24 | 25 | 26 | 27 | 28 |
29 | 30 | |||||
Kalenda ya Gregori |
Tarehe 26 Juni ni siku ya 177 ya mwaka (ya 178 katika miaka mirefu). Mpaka uishe zinabaki siku 188.
Matukio
[hariri | hariri chanzo]- 1945 - Umoja wa Mataifa unaanzishwa mjini San Francisco na kuchukua nafasi ya Shirikisho la Mataifa
- 1960 - Kisiwa cha Madagaska kinapata uhuru kutoka Ufaransa
- 1960 - Somalia ya Kiingereza inapata uhuru kutoka Uingereza
Waliozaliwa
[hariri | hariri chanzo]- 1581 - Mtakatifu Petro Claver, padri mmisionari wa Shirika la Yesu kutoka Hispania
- 1891 - Sidney Howard, mwandishi kutoka Marekani
- 1892 - Pearl S. Buck, mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fasihi mwaka wa 1938)
- 1937 - Robert Richardson, mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fizikia mwaka wa 1996
- 1941 - Omar Ali Juma, mwanasiasa kutoka Zanzibar
- 1942 - Gilberto Gil, mwanamuziki na Waziri wa Utamaduni nchini Brazil
- 1946 - Anthony John Valentine Obinna, askofu Mkatoliki kutoka Nigeria
- 1966 - Adam Kighoma Malima, mbunge wa Tanzania
- 1970 - Sean Hayes, mwigizaji wa filamu kutoka Marekani
- 1987 - Samir Nasri, mchezaji mpira kutoka Ufaransa
Waliofariki
[hariri | hariri chanzo]- 1541 - Francisco Pizarro, aliyevamia Peru na kuharibu Dola la Inka, anauawa mjini Lima
- 1943 - Karl Landsteiner, mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Tiba mwaka wa 1930)
- 1975 - Mtakatifu Josemaría Escrivá, padri, mwanzilishi wa Opus Dei kutoka Hispania
- 2007 - Amina Chifupa, mbunge wa Tanzania
Sikukuu
[hariri | hariri chanzo]Wakristo wengi, wakifuata mapokeo ya Roma, huadhimisha kumbukumbu za watakatifu Yohane na Paulo wa Roma, Vijili wa Trento, Deodati wa Nola, Masensi wa Poitiers, Daudi wa Thesalonike, Salvio na mwenzake, Pelaji wa Cordoba, Rodolfo wa Gubbio, Antelmi wa Belley, Yosefu Ma Taishun, Yosefu Maria Robles, Yosefu Maria Escriva n.k.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu 26 Juni kama enzi zake au matokeo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |