Human Nature
“Human Nature” | |||||
---|---|---|---|---|---|
Single ya Michael Jackson kutoka katika albamu ya Thriller | |||||
B-side | "Baby Be Mine" | ||||
Imetolewa | 3 Julai 1983 | ||||
Muundo | 7" single | ||||
Imerekodiwa | 1982 | ||||
Aina | R&B | ||||
Urefu | 4:06 (toleo la albamu) 3:45 (toleo la single) | ||||
Studio | Epic Records | ||||
Mtunzi | Steve Porcaro John Bettis | ||||
Mtayarishaji | Quincy Jones | ||||
Mwenendo wa single za Michael Jackson | |||||
|
"Human Nature" ni wimbo wa R&B uliombwa na msanii wa rekodi za muziki wa Kimarekani, Michael Jackson. Wimbo huu ulitungwa na Steve Porcaro na John Bettis, na ulitayarishwa na Quincy Jones kwa ajili ya albamu yake ya sita ya Thriller (1982). Awali, Porcaro alirekodi demo kaseti ya majaribio ya wimbo huu, ambayo hiyo ndiyo baadaye alikuja kupewa Jones.
"Human Nature" ulitolewa mnamo tar. 3 Julai 1983, ukiwa kama wimbo wa tano katika albamu. Japokuwa wimbo haujatolewa nchini UK, wimbo ulipata mafanikio makubwa katika chati za US. Kwa kushika namba mbili kwenye chati za Billboard' Hot Adult Contemporary na namba saba kwenye chati za Hot 100. Wimbo huu ni wa tano wa Michael Jackson kutoka katika albamu ya "Thriller" na kuingia kwenye Kumi Bora'. Nchini New Zealand, single ilishika nafasi ya 11. Wimbo huu wa "Human Nature" ulikuja kuimbwa na kusampuliwa na wasanii kibao. Wasanii hao ni pamoja na: Miles Davis, SWV, Nas, Jason Nevins na Boyz II Men.
Chati zake
[hariri | hariri chanzo]Chati (1983) | Nafasi iliyoshika |
---|---|
U.S. Billboard Hot 100 | 7 |
U.S. Billboard R&B Singles chart | 27 |
U.S. Billboard Adult Contemporary chart | 2[1] |
Dutch Singles Chart | 11[2] |
Chati (2009) | Nafasi iliyoshika |
UK Singles Chart | 62[3] |
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Hyatt, Wesley (1999). The Billboard Book of #1 Adult Contemporary Hits (Billboard Publications), page 269.
- ↑ "Dutch Singles Chart Archives". dutchcharts.nl. Iliwekwa mnamo 11 Aprili 2009.
- ↑ "UK Singles Chart". The Official UK Charts Company. Iliwekwa mnamo 6 Julai 2009.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- George, Nelson (2004). Michael Jackson: The Ultimate Collection booklet. Sony BMG.
- Halstead, Craig (2007). Michael Jackson: For the Record. Authors OnLine. ISBN 978-0-7552-0267-6.
- Thriller 25: The Book (2008). Thriller 25: The Book. ML Publishing Group. ISBN 978-0-9768891-9-9.
{{cite book}}
: CS1 maint: numeric names: authors list (link)
Makala hii kuhusu mambo ya muziki bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Human Nature kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |