Nenda kwa yaliyomo

Konventi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Konventi ya Steinfeld huko Ujerumani.
Jiko la konventi huko Ureno.

Konventi ni jumla ya majengo maalumu ya jumuia ya kitawa isiyo ya wamonaki (kanisa, vyumba vya kulala, meza, sebule n.k.).

Konventi, iliyoanza mwishoni mwa Karne za Kati, si tena ngome ya kujitegemea kama monasteri , ambayo kwa kawaida ilikuwa kubwa zaidi kutokana na wingi wa watawa walioikalia na wa kazi walizofanya na huduma walizotoa.

Malengo ya konventi ni hasa malazi ya watawa wanaofanya kazi zao nyingi nje ya nyumba yao, k.mf. Wafransisko na Wadominiko.