Timu ya Taifa ya Zanzibar
Timu ya Taifa ya Zanzibar (maarufu kwa jina la Zanzibar Heroes) inaiwakilisha Zanzibar kwenye mashindano ya kimataifa ya mpira wa miguu na inasimamiwa na shirikisho la mpira wa miguu la Zanzibar.
Historia
[hariri | hariri chanzo]Zanzibar sio mwanachama wa shirikisho la mpira wa miguu Duniani FIFA, hivyo haiwezi kushiriki mashindano ya Kombe la Dunia. Zanzibar ni sehemu ya Tanzania ambayo ni mwanachama wa FIFA katika ngazi za kimataifa. Kabla ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar mwaka 1964, Zanzibar ilikuwa mwanachama wa kujitegemea wa chama cha mpira wa miguu Afrika CAF, lakini haikuwahi kufuzu fainali za Kombe la Mataifa Afrika.
Zanzibar alishawahi kuwa mwanachama wa muda kwenye bodi ya N.F. Walishika nafasi ya pili kwenye mashindano ya FIFI Wild Cup yam waka 2006, wlaipoteza fainali kwa penati 4-1 dhdi ya Timu ya taifa ya Uturuki. Katika michuano hiyo, Oliver Pocher alikua ndiye Kocha wao, anatokea nchini Ujerumani na ni msanii wa vichekesho.
Timu yao ya vijana wa umri chini ya miaka 20 ilishiriki mashindano ya ELF Cup ya mwaka 2006, walimaliza nafasi ya nne kati ya timu nane, walishinda mchezo mmoja tu dhidi ya Krygystan kwa kuwafunga goli 1-0, walitoka sare michezo miwili dhidi ya Gaugazia na Greenland kabla ya kupoteza kwa magoli 5-0 dhidi ya Northern Cyprus hatua ya nusu fainali. Mara kwa mara huwa wanashiriki mashinado ya CECAFA, mashindano haya yanahusisha timu za taifa kutoka Afrika mashariki na Afrika ya Kati na walishinda taji hilo mwaka 1995, waliwafunga wenueji wa mashindano hayo timu ya taifa ya Uganda goli 1-0 kwenye hatua ya fainali.
Mnamo Machi 2017, Zanzibar walipata uanachama wa CAF na kuwa mwanachama wa 55,[1] Uanachama wao ulidumu kwa miezi minne tu, Raisi wa CAF wa kipindi hicho bwana Ahmad Ahmad alitengua uanachama wa Zanzibar kwa madai kwamba uanachama huo haukupaswa kutolewa kwani visiwa vya Zanzibar sio nchi inayojitegemea.[2]
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Zanzibar admitted as full member of African soccer body". indianexpress.com. Indian Express. 16 Machi 2017. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 17 Machi 2017. Iliwekwa mnamo 16 Machi 2017.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Zanzibar loses Caf membership in embarrassing U-turn". bbc.com. British Broadcasting Corporation. 21 Julai 2017. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 23 Julai 2017. Iliwekwa mnamo 23 Julai 2017.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)