Nenda kwa yaliyomo

Wamatumbi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Lindi Manispaa.

Wamatumbi ni kabila la watu wa Tanzania wanaoishi katika Mkoa wa Lindi, wilaya ya Kilwa. Lugha yao ni Kimatumbi.

Wengi wao wanapatikana Kaskazini mwa wilaya ya Kilwa, katika tarafa za Miteja na Kipatimu. Tarafa ya Kipatimu ina eneo kubwa zaidi linalokaliwa na jamii ya kabila la Wamatumbi, ambapo baadhi ya vijiji vyake ni Kipatimu, Namayuni, Chumo na Nandete. Katika tarafa ya Miteja, asili ya Kimatumbi inapatikana zaidi katika kata za Mingumbi na Kinjumbi. Kata za Somanga, Tingi na Miteja ziko ukanda wa pwani ambapo lugha ya Kimatumbi haiongelewi sana. Maeneo hayo yana mwingiliano wa jamii nyingine za wageni wanaokuja kwa ajili ya shughuli za biashara na uvuvi.

Wamatumbi huishi kwa kutegemea kilimo. Ni wakarimu sana na wanaishi kwa kusaidiana na kutegemeana.

Miongoni mwao wapo Wakristo na Waislamu na dini hizo zimeenea kulingana na maeneo ambayo watawala wa zamani yaani wakoloni wamepita. Kwa mfano, kata ya Kipatimu kuna Wakristo wengi kuliko kata nyingine kwa vile wamisionari walijenga makanisa makubwa katika vijiji vya Kipatimu na Nandete. Katika eneo la Kipatimu pia walijenga shule na hospitali.

Makala hii kuhusu utamaduni wa Tanzania bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Wamatumbi kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.