Nenda kwa yaliyomo

Wilaya ya Lugari

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Wilaya ya Lugari ilikuwa wilaya mojawapo ya Mkoa wa Magharibi wa Jamhuri ya Kenya hadi ilipopitishwa katiba mpya ya nchi (2010).

Makao makuu yalikuwa mjini Lugari.

Kwa sasa imekuwa sehemu ya kaunti ya Kakamega.

Wilaya hii imesheheni jamii kadhaa, baadhi yake ni: Tachoni, Maragoli, Banyala, Basoko na zinginezo. Jamii hizi mara nyingi hujihusisha na shughuli za ukulima na biashara.

Baadhi ya mimea inayokuzwa kwa wingi ni:miwa, mahindi, viazi vitamu, ndizi, wimbi, mtama, maharagwe, njugu, ndengu na kadhalika.

Licha ya kwamba wilaya hii haina chuo kikuu, kuna taasisi kadhaa za kielimu zilizianzishwa na hivi karibuni zitaanza kutoa mafunzo mbalimbali ya kitaaluma kwa wasomi punde tu wanapotamatisha masomo yao ya kidato cha nne. Kuna mikakati inaendelea ya kujenga chuo cha kadri katika mji wa Lugari ambacho kitatoa mafunzo ya ualimu hadi kiwango cha diploma. Tayari kuna kimoja kilichokamilika katika mji wa Likiyani nyanda za juu mwa wilaya ya Lugari. Taasisi hii hutoa mafunzo mbalimbali kwa vijana na watu wazima kwa ujumla.

Historia ya wilaya hii kwa ufupi ni kwamba sehemu hii iitwayo Lugari kitambo ilikuwa ikijulikana kama wilaya ya kakamega. Baadaye kwa sababu kakamega ilikuwa sehemu kubwa sana ndiposa ikakawanywa kuwa wilaya mbili, Lugari ya sahi na Malava iliyorudi upande wa Kakamega. Jina lenyewe Lugari linamaanisha mahali ambapo gari la moshi hupita na kusimama. Kulingana na historia wakati wa enzi za ukoloni, reli inayojulikana kama Kenya-uganda railway ilijengwa mwaka wa elfu moja mia tisa na moja. Reli hii ilipita mahali ambapo hivi sasa panajulikana kama mji wa lugari. iwapo utafika katika mji huu, utakunduwa kwamba reli imepita katikati mwa mji huu na kuukawa katika sehemu mbili. Wakati huo wa enzi za ukoloni, gari la moshi lilipita na kupewa jina ligari katika lahaja ya kiluhya. Hili jina lilitokana jina la wakoloni wafanyibiashara- gari la moshi. Kwa hivyo hivi ndivyo baadaye jina Lugari lilipatikana.

Watu wa wilaya hii wana utamaduni mbalimbali kama tohara kwa vijana sherehe inayofanyika kila baada ya miaka miwili kwanzia mwezi wa nane, kwa kiluhya, sherehe hii huitwa okhusevana. Sherehe hii hukamilika mwezi wa desemba pale ambapo vijana waliopashwa tohara hupelekwa mtoni na wazee wa jamii kufunzwa maneno muhimu ya utu uzima na mila za jamii.

Wakati wa sherehe hizi mwanamke au kijana ambaye hajatahiri hawaruhusiwi kuandama na msafara huu kwa sababu ni hatia kubwa kulingana na mila na desturi za waluhya. Iwapo yeyote ataghairi na kupatikana, anaitwa mbele ya kikao cha wazee wa jamii wanaweza kumfanyiya chochote ambacho chaweza kumletea madhara makubwa maishani mwake. Kikao cha wazee wa jamii kinaheshimiwa sana katika jamii ya waluhya maana kuna tetesi kwamba chochote wanachosema hutendeka kwa sababu watu huamini kwamba wana nguvu na uwezo wa kimiungu kutoka kwa waanjilisha wa jamii ya waluhya.

Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Magharibi bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Wilaya ya Lugari kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.