Theta
Mandhari
Alfabeti ya Kigiriki | |||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|
Herufi za kawaida | |||||||
Α α Alfa | 1 | Ν ν Ni | 50 | ||||
Β β Beta | 2 | Ξ ξ Ksi | 60 | ||||
Γ γ Gamma | 3 | Ο ο Omikron | 70 | ||||
Δ δ Delta | 4 | Π π Pi | 80 | ||||
Ε ε Epsilon | 5 | Ρ ρ Rho | 100 | ||||
Ζ ζ Dzeta | 7 | Σ σ ς Sigma | 200 | ||||
Η η Eta | 8 | Τ τ Tau | 300 | ||||
Θ θ Theta | 9 | Υ υ Ipsilon | 400 | ||||
Ι ι Iota | 10 | Φ φ Phi | 500 | ||||
Κ κ Kappa | 20 | Χ χ Khi | 600 | ||||
Λλ Lambda | 30 | Ψ ψ Psi | 700 | ||||
Μ μ Mi | 40 | Ω ω Omega | 800 | ||||
Herufi za kihistoria1 | |||||||
Digamma | 6 | San | 90 | ||||
Stigma | 6 | Sho | 90 | ||||
Heta | 8 | Koppa | 90 | ||||
Sampi | 900 | ||||||
1 Viungo vya Nje: Alfabeti_ya_Kigiriki#Viungo_vya_Nje |
Theta ni herufi ya nane katika Alfabeti ya Kigiriki. Theta kubwa Θ ina umbo la "O" yenye mstari wa katikati. Theta ndogo θ ina umbo la duaradufu nyembamba pamoja na mstari lala wa katikati lakini kuna pia umbo lisilofungwa kama ϑ.
Kwa matumizi ya tarakimu inamaanisha namba 9.[1]
Matamshi yake siku hizi ni sawa na "th" kwa Kiswahili.
Matumizi ya kisayansi
[hariri | hariri chanzo]Jinsi ilivyo kawaida na herufi mbalimbali za kigiriki inatumiwa kama kifupi kwa ajili ya dhana mbalimbali katika hesabu na sayansi. Mifano kadhaa ni
- katika fani ya fizikia
- Theta ndogo θ au ϑ ni alama ya halijoto
- Theta ndogo ni alama kwa kiwango cha pembe katika usokotaji.
- Theta kubwa Θ hutumiwa kama alama ya kuonyesha nguvu ya uga magnetiki
- katika fani ya astronomia
- Theta kubwa Θ inataja saa za nyota
- Theta ndogo ϑ hutaja nyota inayoonekana kwenye nafasi ya tisa katika kundinyota kulingana na nguvu ya nuru yake.